1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Sharon atishia kutoisadia Palestina katika uchaguzi

18 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEZu

Waziri mkuu wa Israel, Ariel Sharon, ametishia kutoisaidia Palestina katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Januari mwakani, ikiwa kundi la wanamgambo wa Hamas litaruhusiwa kushiriki.

Gazeti la New York Times limemnukulu Sharon akisema kwamba Israel inaweza kuamua kuviwacha vizuizi vya barabarani katika ukingo wa magharibi, na kuongeza vingine, hivyo kuwazuilia wapigaji kura wengi kutoweza kuvifikia vituo vya kupigia kura.

Kundi la Hamas limetangaza nia yake ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika uchaguzi na linatarajiwa kupata uungwaji mkono mkubwa. Kundi hilo lilipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mabaraza ya miji mapema mwaka huu huko ukanda wa Gaza.