JERUSALEM :Viongozi wa Israel na Palestina waandaa ratiba ya pamoja ya mkutano
3 Oktoba 2007Viongozi wa Israel na Palestina wanakutana mjini Jerusalem kujaribu kuandaa ratiba ya pamoja ya kikao cha mwezi ujao cha kujadilia amani ya mashariki ya kati.Mkutano huo unafanyika baada ya Israel kuwaachia huru wafungwa 86 kama ishara ya urafiki.Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas wanatarajiwa kuchukua hatua za kwanza muhimu za kufikia makubaliano kabla ya mkutano wa mwezi Novemba na jamii ya kimataifa.
Wakati huohuo watu wane wameuawa katika ghasia katika eneo la Pakistan baada ya gari moja kulipuka karibu na makao makuu ya polisi wa Hamas mjini Gaza.Kulingana na jeshi la Al Aqsa linalohusiana na chama cha Fatah watu watatu kati ya wanne waliofariki walikuwa wapiganaji wa kundi hilo waliouawa walipojibu mashambulizi.Kwa mujibu wa mtandao unaohusika na kundi la Hamas, wapiganaji hao watatu wa Fatah walikuwa wakielekea kulipua eneo la Hamas.Mtu wa nne aliyeuawa alikuwa mpita njia.