1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Viongozi wa Palestina na Israel kukutana.

10 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKk

Viongozi wa Israel na Palestina watakutana siku ya Jumapili kwa mara ya pili katika muda wa mwezi mmoja katika juhudi za kuweka njia yao ya mawasiliano wazi, amesema afisa wa Kipalestina. Lakini pande zote mbili zimekiri jana Ijumaa kuwa hazitarajii mambo makubwa kutokea kabla ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina.

Mkutano huo kati ya waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa Palestina Mahmoud Abbas umepangwa kama sehemu ya juhudi zinazoungwa mkono na Marekani kuzishawishi pande hizo mbili kurejea katika mazungumzo ya amani.

Wakati huo huo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ametangaza mipango ya kuzitembelea Lebanon , Israel na maeneo ya Palestina akiwa njiani kuelekea katika mkutano wa umoja wa mataifa ya Kiarabu baadaye mwezi huu.