1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Jeshi la Israel lafanya mashambulizi dhidi ya Hezbollah

5 Oktoba 2024

Jeshi la Israel limesema vikosi vyake vimewashambulia wapiganaji wa Hezbollah ndani ya msikiti wa kusini mwa Lebanon usiku wa kuamkia Jumamosi (05.10.2024).

https://p.dw.com/p/4lRL1
Jeshi la Israel lafanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Hezbollah kusini mwa Lebanon
Jeshi la Israel lafanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Hezbollah kusini mwa LebanonPicha: Aziz Taher/REUTERS

Hayo ni mashambulizi ya kwanza ya aina hiyo tangu kuanza kwa makabiliano kati ya Israel na wanamgambo hao Oktoba mwaka jana.

Taarifa ya jeshi la  Israel imesema kamandi hiyo Hezbollah iliyokuwa ndani ya nyumba ya ibada ilitumiwa na kundi hilo kupanga na kutekeleza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jeshi na taifa la Israel.

Kwa upande wake kundi la Hezbollah limesema kuwa wapiganaji wake wake walirusha roketi  katika kambi ya jeshi ya Israel ya Ramat David karibu na mji wa kaskazini mwa Israel wa Haifa.

Kwa upande wake, Kundi la Hamas pia limesema Jumamosi kwamba shambulio la Israel dhidi ya kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Lebanon limemuua moja ya viongozi wake, Saeed Atallah Ali pamoja na familia yake.