1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Burkina Faso laangamiza wanamgambo kaskazini

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

Jeshi la Burkina Faso limewaua wanamgambo kadhaa katika operesheni mbili tofauti kwenye maeneo yenye hali tete kiusalama ya kaskazini.

https://p.dw.com/p/4Xl8w
Russland Ibrahim Traore
Rais Ibrahim Traore wa Burkina Faso akizungumza kwenye mkutano na Rais Vladimir Putin wa Urusi (hayupo pichani) mwezi Julai 2023.Picha: Alexey Danichev/AFP

Shirika la habari nchini humo, AIB, limeripoti kwamba karibu wanamgambo 60 walianzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wasaidizi wa kiraia katika kijiji cha Zoura katika jimbo la Bam.

Mashambulizi ya anga pia yalitekelezwa dhidi ya kundi jingine la wanamgambo huko katika jimbo la Silgadji.

Soma zaidi: Mali, Niger, Burkina Faso wanakabiliwa na uasi wa jihadi kwa muda mrefu

Hata hivyo shirika hilo halikubainisha zaidi idadi wa wanamgambo waliouwawa katika oparesheni hiyo.

Vyombo vya habari vya serikali mara kwa mara hutia chumvi operesheni za jeshi dhidi ya makundi ya kigaidi ikiwemo kundi la Dola la Kiislam na matawi ya al-Qaeda ambayo yamevuruga usalama wa Burkina Faso tangu 2015.