1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAsia

Jeshi la China liko tayari kuvunja njama za Taiwan kujitenga

12 Januari 2024

Wizara ya ulinzi ya China imesema kuwa Jeshi la Ukombozi wa Wananchi la nchi hiyo, PLA limejiandaa wakati wote na litachukua hatua zote zinazohitajika kuvunja njama yoyote ya Taiwan kujitenga na kujitangazia uhuru wake.

https://p.dw.com/p/4bA4j
China | Wu Qian bMsemaji wa wizara ya ulinzi
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Wu Qian.Picha: Chen Boyuan/HPIC/dpa/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya China imesema kuwa Jeshi la Ukombozi wa Wananchi la nchi hiyo, PLA limejiandaa wakati wote na litachukua hatua zote zinazohitajika kuvunja njama yoyote ya Taiwan kujitenga na kujitangazia uhuru wake.

Msemaji wa wizara hiyo, Zhang Xiaogang amesema PLA itatetea kwa uthabiti uhuru wa China. Kauli hiyo aliitoa alipoulizwa na waandishi habari kuzungumzia kuhusu hatua ya Taiwan kuboresha ndege zake za kivita na mpango wa ununuzi wa ndege zaidi kutoka Marekani.

Soma pia: Wagombea Urais Taiwan wachuana katika mdahalo kabla ya uchaguzi

China inadai kuwa Taiwan ni sehemu ya himaya yake. Wakati huo huo, maelfu ya wafuasi wa vyama vitatu vya siasa vya Taiwan wataandamana leo wakati ambapo wagombea wanafanya kampeni zao za mwisho kuomba kura kuelekea uchaguzi utakaofanyika kesho ambao China imeonya kuwa unaweza kukitumbukiza kisiwa hicho katika vita.