SiasaIsrael
Jeshi la Israel latoa wito mpya wa kuhama Beirut Kusini
13 Novemba 2024Matangazo
Hii ni mara ya tatu ambapo Israel imetoa onyo kama hilo katika muda wa saa 24.
Eneo hilo la kusini mwa Beirut limeshambuliwa baada ya jeshi la Israel kutoa amri ya watu kuondoka lilitaja eneo hilo kuwa ni ngome ya kundi la Hezobollah.
Picha za chombo cha habari cha AFP zilionyesha moshi mweusi ukifuka katika eneo hilo baada ya kushambuliwa, takriban saa moja baada ya jeshi la Israel kuwaambia wakaazi katika sehemu za vitongoji vya kusini kuondoka.