1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Jeshi la Mali lapeleka jeshi kaskazini kupambana na waasi

4 Oktoba 2023

Jeshi la Mali limepeleka kikosi chake kwenye ngome kuu ya waasi wanaopigania kujitenga kaskazini mwa nchi hiyo kushiriki kwenye operesheni yenye hatari kubwa.

https://p.dw.com/p/4X7Xv
Walinda amani wa MINUSWA wakishika doria nchini Mali
Walinda amani wa MINUSWA wakishika doria nchini MaliPicha: Nicolas Remene/Le Pictorium/MAXPPP/dpa/picture alliance

Oparesheni hiyo huenda ikasababisha makabiliano makubwa na kubadili mwelekeo wa hali ilivyo baada ya muongo mmoja wa mgogoro nchini humo.

Msafara mkubwa wa jeshi la Mali uliondoka mjini Gao siku ya Jumatatu ukielekea katika eneo la  kaskakazini la Kidal.

Imeripotiwa kwamba Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umeondolewa na utawala wa kijeshi na kambi zao kuzikabidhi kwa maafisa wa Mali.

Mji huo wa Kidal ni kituo cha kihistoria cha waasi wanaopigania kujitenga wakiongozwa na jamii ya kabila la Watuareg na mji huo kuendelea kudhibitiwa na waasi  limebakia kuwa suala linalowakasirisha watawala wa kijeshi mjini Bamako.

Jeshi lilipata pigo kwa kushindwa mara nyingi katika mapambano yake na waasi hao kati ya mwaka 2012 na 2014.