1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Jeshi la Mali ladai kukuta kaburi la pamoja, Kidal

19 Novemba 2023

Jeshi la Mali limesema limegundua kaburi la halaiki katika mji wa kaskazini mashariki wa Kidal, uliorejeshwa hivi karibuni kutoka kwa waasi wa Tuareg.

https://p.dw.com/p/4Z91u
Mali | Mwanajeshi akiwa na bunduki aina ya Ak-47
Wanajeshi wa Mali wakishika doria kati ya miji ya Gao na Kidal mnamo Julai 26, 2013, wakati taifa hilo likiwa katika kampeni za urais, siku mbili kabla ya upigaji kura unaoonekana kuwa muhimu katika kurejesha amani katika nchi iliyokumbwa na machafuko ya kisiasa na vita.Picha: KENZO TRIBOUILLARD/AFP/Getty Images

Jeshi hilo la Mali limesema jana jioni kwenye taarifa yake kwamba kaburi hilo la pamoja linaashiria ukatili uliofanywa na magaidi hao ambao hawana imani wala sheria..

Ilisema waligundua kaburi hilo siku ya Alhamisi wakati wa operesheni za kulirejesha eneo hilo la Kidal, ingawa haikutoa maelezo zaidi.

Kulingana na taarifa hiyo, uchunguzi unaendelea ili kuwawajibisha wahusika wa ukatili huo.

Mali iliurejesha mji huo mnamo Novemba 14, ambao ulikuwa ngome ya watu wanaotaka kujitenga wa Tuareg na ambao hawakuwa chini ya udhibiti wa serikali kuu tangu mwaka 2014.