1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMali

Jeshi la Mali lawaua karibu magaidi 40

28 Oktoba 2024

Jeshi la Mali limesema limewauwa takriban magaidi 40 na kuharibu moja ya ngome zao katika operesheni mbili zilizofanyika nchini humo.

https://p.dw.com/p/4mJ8E
Mali Bamako | Mkuu wa majeshi ya Malis Oumar Diarra
Mkuu wa jeshi la Mali Oumar Diarra (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mjini Bamako baada ya Kundi la jihadi lenye uhusiano na Al-Qaeda mnamo Septemba 17, 2024 kudai kuhusika na shambulizi kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi.Picha: ORTM/AFP

Operesheni hizo zilizofanyika Alhamisi na Ijumaa wiki iliyopita ziliharibu ngome katika mji wa Ounguel.

Operesheni ya Alhamisi katika mji huo iliharibu ngome moja na kuwauwa takriban magaidi 30 huku risasi, silaha na pikipiki 24 zikikamatwa, wakati operesheni iliyofanyika Ijumaa ilifanikisha kuuwawa kwa wanamgambo 10 pamoja na kukamatwa bidhaa kadhaa ikiwemo magari na pikipiki.

Mali ambayo inakabiliana na migogoro ya kisiasa, usalama na uchumi imekuwa ikiandamwa na makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na lile linalojiita dola la kiislamu tangu mwaka 2012.