1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Mali limewakamata watu12 wanaodaiwa kuwa magaidi.

25 Aprili 2023

Watu hao walikamatwa kwenye eneo la matata la kaskazini mashariki ambako wapiganaji wanaohusiana na kundi linalojiita dola la kiislamu limepanuza wigo wa sehemu wanayodhibiti.

https://p.dw.com/p/4QW1k
Symbolbild Islamisten in Burkina Faso
Picha: ROMARIC OLLO HIEN/AFP/Getty Images

Jeshi la Mali limewakamata watu12 wanaodaiwa kuwa magaidi. Watu hao walikamatwa kwenye eneo la matata la kaskazini mashariki ambako wapiganaji wanaohusiana na kundi linalojiita dola la kiislamu limepanuza wigo wa sehemu wanayodhibiti. Hata hivyo waasi wa zamani wa kitaureg wamesema wapiganaji hao ni wa kwao. Msemaji wa waasi hao wa zamani ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watu hao waliokamatwa siyo magaidi. Msemaji huyo ameeleza kuwa watu hao ni askari wa waasi wa hapo zamani waliomo katika jeshi la Mali ambalo limeundwa upya. Kwa mujibu wa taarifa makubaliano ya amani yalitiwa saini kati ya waasi na serikali mnamo mwaka 2015 lakini utekelezaji wake ulisimamishwa kutokana na mivutano baina ya utawala wa kijeshi na makundi kadhaa. Jeshi la Mali pia limefahamisha kwamba magaidi 29  waliuliwa katika mashambulio yaliyofanywa na ndege.