Marekani yapiga zaidi ya vituo 85 vya wanamgambo Syria, Iraq
3 Februari 2024Shirika la uangalizi wa haki za binadamu nchini Syria, lenye makao yake nchini Uingereza, limesema katika taarifa kwamba ndege za kivita za Marekani zimefanya duru kadhaa za mashambulizi dhidi ya maeneo kwenye urefu wa kilomita 130 kuanzia mji wa Deir e-Zour hadi mpaka wa Syria na Iraq.
Soma pia: Biden aamua kujibu shambulizi lililotokea Jordan
Shirika hilo limesema wanamgambo wasiopungua 18 wanaoiunga mkono Iran wameuawa. Kamandi ya kanda ya jeshi la Marekani, CENTCOM, imethibitisha mashambulizi hayo kupitia mtandao wa X, na kusema maeneo yalioshambuliwa ni pamoja na vituo vya kamandi na udhibiti wa operesheni, intelijensia, hifadhi za maroketi, makombora na droni miongoni mwa vingine.
Ikulu ya White House imesema Marekani hatitaki vita na Iran licha ya mashambulizi hayo.