Jeshi la Uingereza liliuwa kwa makusudi Afghanistan
8 Januari 2025Matangazo
Mmoja wa wanajeshi hao aliiambia tume hiyo kwamba aliwahi kulielezea suala hilo kwa wakubwa zake tangu mwaka 2011, ambapo aliweka wazi kwamba wanajeshi wa Uingereza waliuawa vijana hadi wa miaka 16, ambao hawakuwa kitisho chochote kwa usalama wao.
Katika tukio moja, Kikosi Maalum cha Jeshi la Anga la Uingereza, SAS, kiliwauwa watu 54 kwa wakati mmoja.
Soma zaidi: Urusi yaitaka Magharibi kuindolea vikwazo Afghanistan
Kwa mujibu wa wanajeshi hao, waliamriwa kwenye operesheni hiyo, waliamriwa kuwalenga wanaume wote wenye umri wa kupigana bila kujali kama walikuwa wanamgambo ama la.
Tume hiyo imechapisha sehemu ya kwanza ya uchunguzi wake hivi leo ikiweka hadharani ushahidi wa wanajeshi saba, ambao haikuwataja majina.