Jinsi kalunguyeye, ndege na panya wanavyoishi kwenye majira ya baridi
Je, wanyama wadogo wenye miguu dhaifu wanaishi vipi kwenye majira ya baridi kali, wakati tunapotetemeka licha ya kuwa tunavalia mavazi maalum, viatu na glovu? Wanyama hawa hutumia mbinu kadha wa kadha.
Kwanini miguu yao si baridi?
Miguu midogo ya ndege — kama ile ya greenfinch — haipiti urefu wa milimita mbili. Wanawezaje kuwa kwenye barafu siku nzima, kwenye halijoto ya kiwango cha chini, wakati ambapo tayari vidole na miguu yetu inakufa ganzi kwa baridi?
Kinga ya ndani dhidi ya baridi
Ndege wana mishipa ya kudhibiti halijoto. Mishipa hiyo hukinga miguu yao dhidi ya barafu, wakati wanapotembea kwenye theluji. Damu husambaa kupitia mishipa yao ya damu iliyosukwa kama wavu hadi miguuni na kupitisha joto kisha ile damu ikarejea mwilini. Kupitia njia hii, damu kwenye miguu ni baridi,lakini mwili haupotezi joto jingi.
Ndege wenye mfumo wa kuzima joto
Kama tu kwenye jengo, mfumo huu unaweza kuzimwa wakati wa joto. Kisha miguu inatoa joto ziada, kwani ndege hawana uwezo wa kutoa jasho kwasababu ya manyoya. Wakati wa majira ya baridi, ni muhimu kwao kupata chakula cha kutosha ili kuhifadhi nishati kwenye miili yao. Almuradi, theluji sio nyingi sana, watapata kitu cha kula.
Nishati tosha kwa ndege wadogo waimbao
Wakati kuna theluji nyingi, wanadamu wanaweza kusaidia, ndege aina ya blue tit na kurumbiza hula chakula chao maalum kinachojumuisha mbegu na nafaka zilizoambatanishwa na mafuta. Kuna nishati kiasi kikubwa katika hilo! Sababu nyingine ambayo ndege hawahisi baridi ni manyoya yao. Huwalindakama majaketi yanavyowalinda wanadamu.
Hupendelea maji ya barafu
Nguo yake ya manyoya inajumuisha kinga ambayo ni hewa nzito inayozuia baridi. Zumbulu hawezi tu kupaa angani, lakini pia kwenye maji ya barafu. Yeye hupenda kusaka mawindo yake kwenye maji yasiyo na barafu wakati wa majira ya baridi. Lakini inamuia vigumu ndege huyo wa kupendeza kwenye maji ambayo hayana samaki wadogo wa kutosha.
Hujificha katika rundo la matawi
Kalunguyeye hula zaidi katika majira ya joto kwa matumaini ya kuwa na hifadhi ya kutosha ya mafuta katika majira ya baridi. Mahali pao pazuri pa kujificha ni kwenye matawi mengi ambayo yatamkinga dhidi ya barafu. Ukiwaona kalunguyeye wadhaifu ama wagonjwa wakati wa majira ya baridi, wasiliana na mtunzi wa wanyama aliyekaribu. Kabla ya kuteketeza matawi angalia ikiwa wapo ndege hao!
Ni vigumu kuwapata wakati wa majira ya baridi
Panya huyu huingia chini ya ardhi majira ya baridi. Atachimba kina cha mita moja chini ya ardhi. Wakati anapojificha, anaishi kwa kutumia hifadhi ya mafuta yake, aliyokusanya wakati wa majira ya joto. Panya huyu hupunguza mapigo ya moyo wake kutoka 300 kwa dakika hadi tano kwa dakika. Hali joto ya mwili wake hupungua kwa takriban nyuzi tano.
Jaa la taka, nyumbani
Panya wanapenda kuishi karibu na binadamu-kama kuishi karibu na jaa la takataka. Halijoto pale huwa juu zaidi ya kuwa barafu. Uzuri mwingine ni kuwa kuna chakula kingi cha kutosha. Majira ya baridi hata maganda ya karoti ni bora kuliko kukosa kitu.
Kupakata kupata joto
Popo hujificha kwenye mapango chini ya majengo. Hapo hujenga makundi na kupeana joto. Hupunguza halijoto ya miili yao kuwa juu kidogo ya mazingira yao. Vitendo vya kujamiiana hufanyika kwenye robo ya majira ya baridi, lakini uunganishaji wa mbegu za kike na kiume mwilini hufanyika wakati wa joto tena. Wakati wanapopo wanazaliwa ni majira ya joto tena.
Usisumbue
Mamalia wakubwa kama paa ama nguruwe mwitu ambao hawajifichi, lazima watafute chakula cha kutosha kuishi kwenye majira ya baridi. Hiyo ina maanisha kuwa wanahitaji kuhifadhi nishati na kuwa hawafai kutembea sana. Usumbufu unaweza kuwa hatari kwao.Ukiwaona wanatembea msituni, kaa mbali na wao pamoja na mbwa wako.
Usisonge
Vyura hawa wawili wamekaa katika barafu iliyoanguka — lakini hawatakaa hapo kwa muda mrefu. Mara nyingi reptilia na amfibia watatafuta ulinzi chini ya miti ama mapango madogo ama kuta zilozopasuka. Hapo watajificha wakiwa na halijoto ya kiwango cha chini.
Si wakati mzuri wa nzi wengi
Nzi wengi hawatajitokeza na kujificha katika mashimo madogo ya mbao, chakula cha farasi ama kwenye miamba. Pengine mbu pekee ndio hawajifichi. Mayai yao yanaweza kuishi kwenye maji ya barafu. Hata katikati ya majira makali ya baridi utawaona mbu wengine. Mara nyingi kwenye makazi ya binadamu, utakuta maji ambayo wadudu hao wanaweza kutaga mayai yao.