Historia ya ukoloni wa Ujerumani ni jambo geni miongoni mwa raia wengi wa taifa hilo. Lakini kwenye miji kadhaa ya Ujerumani zipo kumbukumbu na alama kuhusu ukoloni wa nchi hiyo. Nyingi kati ya hizo zilizitengenezwa kuonesha upinzani wa ukoloni. Mwandishi wa DW Lennart Attenberger ameitembelea miji miwili ya Ujerumani kutusimulia historia ya sanamu na alama hizo.