John Bolton akosolewa na baraza la senet la Marekani
12 Aprili 2005Matangazo
Washington:
Mteule wa rais George W. Bush atakaekua balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa John Bolton amekumbwa na lawama kali za maseneta wa nchi hiyo.Wajumbe wa kamisheni ya baraza la Senet wanamlaumu mwanasiasa huyo kwa kushindwa kuithamini vya kutosha jumuia hiyo ya kimataifa na kuikejeli.John Bolton anaifanyia kazi wizara ya mambo ya nchi za nje akishughulikia mipango ya kuzuwia kusambazwa silaha za maangamizi.Wapinzani wake wanahoji ametumia vibaya ripoti za idara ya upelelezi ili kukamilisha malengo yake ya kisiasa.Kabla ya kuidhinishwa na baraza la Senet John Bolton atabidi kwanza aidhinishwe na kamati hiyo ya utafiti .