1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la Urusi laua watu 14 Odesa, Ukraine

15 Machi 2024

Mamlaka nchini Ukraine imetoa ripoti kupitia mitandao ya kijamii kwamba kuwa watu 14 wameuawa katika shambulizi la Urusi kwenye mji wa bandari wa Bahari Nyeusi wa Odesa huku makumi ya wengine wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4dgVU
Ukraine- |  Odesa
Picha inayoonyesha uharibifu uliofanywa na shambulizi la Urusi katika mji wa Odesa uliopo kusini mwa UkrainePicha: Ukrainian Emergency Service Office/AP Photo/picture alliance

    
Watu 14 wameuawa katika shambulizi la kombora lililofanywa na Urusi kwenye mji wa kusini mwa Ukraine wa Odesa mapema hii leo. Hayo yamejiri wakati jopo la uchunguzi ya Umoja wa Mataifa limetoa ripoti leo Ijumaa inayosema Urusi imefanya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa wafungwa wa kivita wa Ukraine.

Soma zaidi: Uchaguzi nchini Urusi unafanyika ikiwa katika vita na Ukraine

Mamlaka nchini Ukraine imetoa ripoti kupitia mitandao ya kijamii kwamba kuwa watu 14 wameuawa katika shambulizi la Urusi kwenye mji wa bandari wa Bahari Nyeusi wa Odesa  huku makumi ya wengine wamejeruhiwa.

Gavana wa mji wa Odesa, Oleg Kiper amesema miongoni mwa watu waliouawa ni wakaazi wa eneo hilo, daktari na muokoaji, watu wengine wakiwemo wafanyikazi saba wa Huduma ya Dharura ya Jimbo hilo, wamejeruhiwa.

Ukraine Odessa
Waokoaji wakisaidia kutoa miili ya waathirika kwenye eneo liloshambuliwa na Urusi katika mji wa Odesa, UkrainePicha: REUTERS

Jopo: Urusi imekiuka sheria za kimataifa

Wakati shambulizi hilo likiripotiwa huko Kusini mwa Ukraine, Jopo la uchunguzi la Umoja wa Mataifa limetoa ripoti yake hii leo ambaye imeinyooshea kidole Urusi ikisema nchi hiyo imetekeleza uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa raia wa Ukraine.

Akiwasilisha ripoti hiyo mjini Geneva, mwenyekiti wa jopo hilo Erik Mose amesema ´´tume imechunguza kesi ziada za mateso yaliyofanywa na mamlaka za  Urusi. Wakati uchunguzi huo unafanyika , tume imezingatia kesi za mateso katika vituo 11 vya kuwashikilia watu,  saba katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Urusi nchini Ukraine na vinne ndani ya Urusi. Waathirika ni wanaume na wanawake, wengi wao wakiwa wanaume wenye umri wa miaka 21 hadi 58´´.

Soma zaidi: Umoja wa Ulaya waonya juu ya mustakabali wa vita vya Ukraine

Ripoti hiyo imewasilishwa mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 47 ambalo litaamua katika kikao chake kinachoendelea mjini Geneva, iwapo muda wa jopo kazi hilo utaongezwa kwa mwaka mwingine mmoja ili kuendelea kufanya uchunguzi zaidi.

Erik Mose
Erik Mose ameogoza jopo la uchunguzi la Umoja wa Mataifa juu ya uva,izi wa Urusi nchini Ukraine.Picha: Igor Burdyga/DW

Kwa upande wake mjumbe wa jopo hilo la Umoja wa Mataifa Vrinda Grover akiwasilisha matokeo ya ripoti hiyo alisema ''Mamlaka ya Urusi ilikiuka sheria za kimataifa za kibinadamu na kufanya uhalifu wa kivita wa kunyakua mali ya adui. Zaidi ya hayo, jopo lilichunguza matukio ya ubakaji na unyanyasaji mwingine wa kingono uliofanywa dhidi ya wanawake katika mazingira ambayo pia ni mateso''.
Hata hivyo, Urusi imeyakanusha madai hayo yaliyotolewa na jopo hilo.

Scholz amkaribisha Macron mjini Berlin

Kwingineko mjini Berlin,Mkutano wao unafuatia matamshi ya Macron aliyoyatoa majuma kadhaa yaliyopita, akipendekeza uwezekano wa kutumwa wanajeshi wa mataifa ya magharibi nchini Ukraine

Olaf Scholz na  Emmanuel Macron
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amemkaribisha rais wa Ufaransa Emmauel Macron mjini Berlin kuijadili UkrainePicha: Lewis Joly/AP/picture alliance

Pendekezo hilo linapingwa vikali na baadhi ya viongozi wa ulaya ikiwemo kansela Scholz. 

Baada ya mkutano wao wa wazi, wawili hao wataungana na Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk kwa mashauriano ya haraka ya namna ya kuisaidia Ukraine.

Ukraine kwa sasa inakabiliwa na msururu wa vikwazo katika uwanja wa vita ikiwemo msaada wa Marekani wa dola bilioni 60 za kimarekani ambao bado umezuiliwa katika bunge la Congress na warepublican wa mrengo wa kulia.