1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juba: Watu 16 wakiwemo watoto wameuawa kufuatia mapigano

17 Januari 2018

Watu 16 wameripotiwa kuuawa ikiwa ni pamoja na watoto watatu, tokea Sudan Kusini kusitisha mapigano chini ya mwezi mmoja uliopita

https://p.dw.com/p/2qyr6
Konflikt im Südsudan Regierungssoldat 31.12.2013
Picha: Samir Bol/AFP/Getty Images

Watu kumi na sita wameripotiwa kuuawa ikiwa ni pamoja na watoto watatu, tokea Sudan Kusini kusitisha mapigano chini ya mwezi mmoja uliopita. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa mara nne tofauti na kundi linalosimamia kusimamishwa mapigano na hatua za mpito za kiusalama uliochapishwa jana Jumanne, vikosi vya serikali na vile vya upinzani vimelaumiwa kwa kukiuka kwa mara kadhaa makubaliano ya kusitisha vita tangu yalipoanza mnamo tarehe 24 mwezi Desemba mwaka uliopita.

Kundi hilo limesema vifo vya watu hao 15 ni vya kusikitisha.

Ripoti hiyo inasema watoto bado wanaendelea kutumika kama wanajeshi na unyanyasaji wa kijinsia bado ungali upo.  Upinzani nchini Sudan Kusini unashutumiwa kuhusika na shambulio la mji wa Koch, masaa machache baada ya kutekelezwa makubaliano hayo ya kusitisha mapigano.

Vikosi vya serikali navyo vishutumiwa kupora mali za  raia na kuchochea vurugu katika mji wa Mundri. Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo vimeingia mwaka wake wa tano, huku maelfu ya watu wakiwa wameuawa, wengi wakiwa katika hali mbaya ya njaa na wengine kupoteza makaazi yao.