Julia Assange aruhusiwa kukata rufaa Uingereza
24 Januari 2022Mahakama kuu mjini London leo imempa haki mfichuzi huyo wa nyaraka za siri za Marekani ya kwenda kukata rufaa ya kuupinga uamuzi wake wa mwanzo uliotaka mwasisi huyo wa Wiki Leaks akabidhiwe kwa Marekani.
Rafiki wa Assange Stella Moris baada ya uamuzi huo aliseam kilichotokea mahakamani ndicho walichokitarajia.
"Kilichotokea mahakamani leo ndicho haswa tulichotaka kitokee. Mahakama kuu imejiridhisha kwamba tuliibua hoja ya kisheria yenye umuhimu kwa uma kwa ujumla na kuona kwamba mahakama ya juu zaidi ina sababu nzuri za kusikiliza rufaa hii,'' alisema Stella Moris.
soma zaidi: Hatma ya Assange kuamuliwa Uingereza
Mahakama ya chini ya Uingereza awali ilitowa uamuzi wa kukataa kumkabidhi Assange kwa Marekani ikisema Assange huenda akajiua akipelekwa katika mazingira magumu ya jela nchini Marekani.
Mahakama ya juu lakini mwezi uliopita iliubatilisha uamuzi huo wa mahakama ya chini,ikisema ahadi zilizotolewa na Marekani zinatosha kuhakikisha Assange hatojidhuru katika jela za Marekani.