Matangazo
Vuguvugu hilo lilipata ushindi wa viti 330 kati ya viti 500 na linataka lipewe nafasi ya uwaziri mkuu na kuunda baraza la mawaziri.
Mwandishi wetu, Saleh Mwanamilongo, amefanya mahojiano maalum na Julien Paluku, aliyekuwa gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini ambaye hivi sasa ni mbunge na mmoja wa viongozi wa vuguvugu hilo.
Paluku ametangaza kujiuzulu kwenye wadhifa wake wa ugavana na kusema hatagombea tena muhula mwingine. Kwanza anaelezea lengo la mazungumzo yao na Rais Mstaafu Kabila mjini Kinshasa.
Mwandishi: Saleh Mwanamilongo
Mhariri: Mohammed Khelef