1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Wito watolewa kuanzishwa mazungumzo nchini Sudan

19 Januari 2024

Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Marekani zimetoa wito wa usitishwaji mapigano na kuanzishwa majadiliano baina ya pande hasimu nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4bRYz
Mamilioni wakimbia Sudan kwa hofu ya mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF
Moshi ukifuka wakati wa mapigano katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, Mei 3, 2023. Mapigano kati ya majenerali wawili nchini humo yamesababisha maafa makubwa na janga la kibinaadamuPicha: AFP

Jamii hiyo ya kimataifa aidha, imetoa wito wa kukomeshwa kwa hali ya wasiwasi kati ya Somalia na Ethiopia kufuatia makubaliano yaliyosainiwa kati ya Addis Ababa na jimbo la Somaliland lililojitenga na Somalia.

Wawakilishi wa pande hizo tatu walitowa kauli hiyo baada ya kukutana na wenzao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Kampala, Uganda, wakisema kuwa migogoro hiyo miwili inatishia usalama wa Pembe ya Afrika.

Pande hizo tatu, pamoja na Umoja wa Mataifa, zinasema mapigano yanayoendelea nchini Sudan yamewalazimisha raia milioni saba kuwa wakimbizi, huku watoto milioni 19 wakishindwa kuhudhuria masomo yao.

Somalia imesema wanatambua mamlaka ya taifa hilo na kutaka kuheshimiwa kwa mipaka yake, na kuashiria umuhimu wa mzozo wake na Ethiopia kumalizwa kwa mazungumzo.