Kagame akubali kutumwa ndege zisizo rubani DRC
22 Januari 2013Matangazo
Baraza hilo linapaswa kufafanua ni kwa jinsi gani ndege hizo zitakomesha vitendo vya usalama mdogo kwenye eneo hilo. Rais Kagame ameyasema hayo kwenye kikao na waandishi wa habari mjini Kigali.
Mapema mwezi huu baraza hilo lilipendekeza kutumwa ndege zisizo na rubani mashariki mwa Kongo lakini Rwanda ililipinga pendekezo hilo ikiomba kuwepo maelezo ya kutosha juu ya azimio hilo. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Sylivanus Karemera
Mtayarishaji: Grace Kabogo
Mhariri: Josephat Charo