Wanaokamatwa ni wanajeshi na waandishi wa habari
27 Julai 2016Taarifa hiyo iliyokaririwa na shirika la habari la Dogan la nchini Uturuki inasema idadi hiyo ndogo ya askari walioshiriki katika jaribio la kuipindua serikali inathibitisha kwamba sehemu kubwa sana ya wanajeshi walizipinga njama hizo.
Tamko la jeshi la Uturuki pia limefahamisha juu ya zana za kijeshi zilizotumika wakati wa jaribio la kuiangusha serikali.
Waasi walitumia ndege 35, ikiwa pamoja na 24 za kivita.Pia walitumia helikopta 37 na saba kati ya hizo zilikuwa za kufanyia mashambulio.Jeshi la Uturuki pia limesema katika taarifa kwamba vifaru 74, magari mengine ya kijeshi na manowari tatu zilitumika katika jaribio.Jeshi la Uturuki lenye wanajeshi wapatao 680,000 ni la pili kwa ukubwa katika jumuiya ya NATO.
Wakati huo huo hati za kuwezesha kukamatwa kwa watu zaidi zilitolewa nchini Uturuki. Kwa mujibu wa habari, hati hizo zimewalenga maafisa 47 wa zamani na waandishi wa habari waandamizi wa gazeti linaloitwa "Zaman" kwa madai kwamba watu hao wanayo mawasiliano na kiongozi wa kidini Fethullah Gulen anaeishi uhamishoni nchini Marekani.
"Gulen ndiye kiranja wa jaribio"
Guleni anatuhumiwa kuwa ndiye alieundaa mpango wa kuipundua serikali. Shirika la habari la serikali,Anadolu limeripoti kwamba aliekuwa mwandishi wa makala, wa gazeti la "Zaman " amewekwa kwenye kuzuizi cha nyumbani.
Gazeti hilo linalotuhumiwa kuhusiana na vugu vugu la Kiongozi wa kidini, Gulen lilivawiwa na polisi na kuzuiwa kufanya kazi mnamo mwezi wa Machi.Mapema wiki hii waandishi habari wengine 42 walikamatwa na 16 miongoni mwao waliwekwa mahubusi kwa ajili ya kuhojiwa.
Kwa mujibu wa habari mpaka sasa watu zaidi ya 13, 000, hasa kutoka jeshini, wametiwa ndani nchini Uturuki tangu kufanyika jaribio la kuipindua serikali.Wakati huo huo askari wa Uturuki waliokimbilia Ugiriki wanafanya matayarisho ya kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini humo.
Wakili wao amesema Hahn amesema hali inabadilika badilika nchini Uturuki .Watu wanasubiri kuona iwapo adhabu ya kifo itarudishwa .Wakili huyo anaewatetea askari wanneamesema kuwa wanajeshi hao wanaogopa kurejea nchini Uturuki kwa sababu wamemwambia kuwa watateswa ikiwa watarudi nchini huko.
Mwandishi:Mtullya abdu,dpa/afp
Mhariri:Yusuf Saumu