SiasaMarekani
Kamati ya Bunge la Marekani yatoa ripoti juu ya uvamizi
23 Desemba 2022Matangazo
Ripoti hiyo yenye kurasa 814 imeutaja uvamizi huo ''usiofikirika'' dhidi ya bunge hilo uliofanywa na wafuasi wa rais aliyeshindwa katika uchaguzi, Donald Trump.
Ripoti hiyo imetoa maelezo kuhusu juhudi za Trump kubatilisha uchaguzi wa rais wa 2020 na imetaja mapendekezo 11 kwa Bunge la Marekani na watendaji wengine kuzingatia ili kuimarisha taasisi za nchi hiyo dhidi ya majaribio ya matukio ya baadae kuhusu kuchochea uasi.
Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kumzuia Trump kuwania tena urais. Kamati hiyo inatoa pia nakala kadhaa za maelezo ya mashahidi kutokana mahojiano yake zaidi ya 1,000 na maelezo mapya ya kushangaza.
Wiki hii, kamati hiyo ilipendekeza rais huyo wa zamani afunguliwe mashtaka ya uhalifu.