1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamati ya Bunge yataka rais Bolsonaro ashitakiwe

21 Oktoba 2021

Kamati ya bunge ya Brazil imesema Rais Jair Bolsonaro anapaswa kushtakiwa kwa makosa tisa ya uhalifu yenye kuhusiana na namna taifa hilo lilivyoshughulikia janga la virusi vya corona na kusababisha watu wengi kufa

https://p.dw.com/p/41wfC
Brasilien | Coronavirus | Vila Formosa Friedhof in Sao Paulo
Picha: Marcello Zambrana/AA/picture alliance

Mwenyekiti wa jopo la kamati ya uchunguzi, Seneta Renan Calheiros jana jioni aliwasilisha ripoti ya mwisho iliyohusu sera ya serikali ya Bolsonaro katika kuabiliana na janga la virusi vya corona baada ya uchunguzi uliodumu kwa miezi sita. Hata hivyo kinakachofauta baada ya hatua hiyo bado hakijawa wazi.

Aidha ripoti hiyo imesema kando na Bolsonaro, watu wengine 65 na wafanyabiashara wawili pia wanapaswa kukabiliwa na mashtaka kutokana na matendo yao ambayo  yalichangia taifa hilo kushika nafasi ya pili kwa idadi ya vifo vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19 duniani.

Ukaidi wa Rais Bolsonaro katika kukabiliana na janga la virusi vya corona.

Jair Bolsonaro
Rais Jair Bolsonaro wa BrazilPicha: Mateus Bonomi/AA/picture alliance

Bolsonaro amekuwa akipuuza athari za virusi vya corona tangu kuanza kwa janga hilo na alikuwa akipinga hatua za kujikinga na kuonesha mashaka na matumizi ya chanjo. Amekuwa akisisitiza mara kadhaa kwamba hata chanjo hajashiriki. Zaidi Senena Renan Calheiros alisema "Uchunguzi wa tume hii ya bunge kuhusu janga, umekusanya ushahidi unaonesha kwamba serikali ya shirikisho ilikuwa kimya na kuchagua kuchukua hatua zisizo za kitaalamu na za kizembe katika kukabilina na janga jipya la virusi vya corona." 

Jopo hilo la maseneta 11 lilikuwa likichunguza kama katika kipindi hiki cha janga la virusi vya vitendo vya Bolsonaro vilichangia vifo vya zaidi ya raia 600.000 nchini Brazil. Katika ripoti hiyo yenye kurasa 1,200, Calheiros ameonesha uwepo wa mashtaka yakiwo ya kusema uongo, matumizi mabaya ya fedha za umma pamoja uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

Rais alitoa msisitizo wa tiba iliyo na mashaka kwa ugonjwa wa Covid-19.

Ripoti inasema kwa kile kilichobainika kwa wakati ule, kusisitiza baadhi ya madawa kama ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria kama vile, hydroxycloloquine ikielezwa kuwa tiba za awali, kwa sera ya serikali katika kukabiliana na janga la virusi vya corona, Bolsonaro alichangia kusambaza maradhi ya Covid-19 katika taifa lake, na kwa hivyo anapaswa kuwajibika kwa makosa alioyafanya.

Baada ya ripoti hiyo Rais Bolsonaro mwenyewe alijitokeza hadharani na kuipinga akisema kuwa ni ya kisiasa yenye lengo la kumuhujumu, na kuongeza kwamba hajafanya kosa lolote.

Lakini ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali, Jenerali Augustino Aras imesema, itaifanyia tathimini ya kina ripoti hiyo pale itakapowafikia, ingawa pia wadadisi wanasema kwa Aras, bado haijawa wazi kama mwendesha mashtaka huyo atakuwa na uwezo wa kumshtaki rais hata kama kutakuwa nguvu ya kisheria ya kufanya hivyo na kwamba zaidi ripoti hiyo itatoa msukumo kwa Bolsonaro kuwania tena urais katika uchaguzi wa 2022 na kumuepusha na mikono ya sheria.

Chanzo: AP