1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Kisa kipya cha homa ya Marburg charipotiwa

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKT

Kisa kipya cha homa ya Marburg kinaripotiwa kutokea katika eneo la magharibi mwa Uganda ikiwa ni miezi miwili tangu ugonjwa huo kudhibitiwa.Kwa mujibu wa Wizara ya Afya mfanyikazi mmoja wa migodi aliingia kwenye mgodi mmoja uliopigwa marufuku.Mgodi huo uko katika eneo linalopakana na Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo kulikoibuka ugonjwa huo mwezi Agosti.Ugonjwa huo ulisababisha kifo cha mtu mmoja wakati huo.Kulingana na wanasayansi chanzo cha virusi hivyo ni popo anayepatikana kwenye eneo la kusini mwa jangwa la Afrika.Homa ya Marburg inasambazwa kwa damu,kinyesi,matapishi,mate,jasho na hata machozi.

Hakuna chanjo au dawa yoyote inayotibu ugonjwa huo unaosababisha kuvuja damu kwenye viungo vya ndani na kusababisha kifo baada ya wiki moja.