1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampuni ya chipu ya Taiwan kufungua kiwanda Ujerumani

8 Agosti 2023

Kampuni ya inaotengeneza vipande vya nyenzo za kieletroniki ya Taiwan TSMC inapanga kujenga kiwanda cha vifaa vya kupitishia umeme kwenye nyezo hizo za kielektroniki katika jiji la mashariki mwa Ujerumani la Dresden.

https://p.dw.com/p/4UvHD
Samsung na Intel
Chipu ya silikoni ya Intel kwa ajili ya SamsungPicha: Mustafa Ciftci /AA/picture alliance

Kampuni ya inaotengeneza vipande vya nyenzo za kieletroniki ya Taiwan TSMC inapanga kujenga kiwanda cha vifaa vya kupitishia umeme kwenye nyezo hizo za kielektroniki katika jiji la mashariki mwa Ujerumani la Dresden kwa uwekezaji utakaogharimu jumla ya dola bilioni 3.8.

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck amekaribisha uamuzi huo wa Taiwan. Taarifa juu ya mradi huo ilitolewa Jumanne baada ya mkutano wa bodi ya kampuni hiyo ya Taiwan. Shughuli za uzalishaji zinatarajiwa kuanza mnamo mwaka 2027. Ujerumani imekubali kudhamini gharama za ujenzi kwa euro bilioni 5.

Hata hivyo umoja wa Ulaya utatoa uamuzi wa mwisho juu ya udhamini huo wa ruzuku. Kampuni ya Taiwan TSMC ambayo ni mzalishaji mkubwa wa vipande vya nyenzo za kielektroniki duniani inapanga kuzalisha nyenzo hizo kwa ajili ya sekta ya viwanda vya magari.