1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Kampuni ya magari ya Volkswagen yapanga kufunga viwanda 3

28 Oktoba 2024

Kampuni ya magari ya Ujerumani ya Volkswagen inapanga kufunga viwanda vyake takriban vitatu ndani ya Ujerumani na kupunguza maelfu ya nafasi za ajira.

https://p.dw.com/p/4mJqe
Volkswagen  yapanga kufanya mageuzi
Picha hii ya Julai 12, 2013 ikionyesha wafanyakazi katika kiwanda cha Volkswagen wakiwa kazini.Picha: Erik Schelzig/AP Photo/picture alliance

Kampuni hiyo pia inapanga kupunguza shughuli katika viwanda vyake vitakavyobakia katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Ulaya, katika mpango wake wa kufanya mageuzi.

Hayo yameelezwa leo na mkuu wa baraza la usimamizi wa shughuli za kampuni hiyo ya utengenezaji magari, Daniela Cavallo.

Kwa wiki kadhaa kampuni ya Volkswagen imekuwa kwenye mazungumzo na vyama vya wafanyakazi kuhusiana na mipango yake ya mageuzi na kupunguza gharama, ikiwemo kufikiria kwa mara ya kwanza kufunga baadhi ya viwanda vyake nchini Ujerumani.

Kampuni ya Volkswagen imeajiri takriban wafanyakazi 300,000 nchini Ujerumani na imekuwa ikikabiliwa na shinikizo, kupunguza gharama zake na kuendelea kuwa na ushindani katika wakati ambapo mahitaji ya bidhaa zake yamepunguwa China na Ulaya