KANO : Polisi 12 wauwawa Nigeria
17 Aprili 2007Matangazo
Polisi 12 wa Nigeria wameuwawa leo hii wakati kundi la watu wasiojulikana lenye silaha walipovamia na kukikalia kituo chao cha polisi katika mji wa kaskazini wa Kano.
Afisa aliekuwepo katika patashika hiyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kundi hilo likijumuisha wanaume na wanawake lilikishambulia kituo hicho cha polisi cha kitongoji wakati wa mchana na kuuwa mkuu wa kituo, mke wake na maafisa 11 wa polisi.
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Nigeria ameweza kuthibitisha kwamba waliokufa ni watano tu na washambuliaji walikuwa watu wa itikadi kali.