Kansela Merkel afanya mazungumzo ya simu na Wen Jiabao
16 Februari 2008Matangazo
BERLIN
Ujerumani na China zimekubaliana kushirikiana kuimarisha uhusiano wao wa kiuchumi na kutembeleana katika pande zote.Uhusiano huo baina ya nchi hizo mbili ulikuwa katika hali mbaya baada ya Kansela Angela Merkel kukutana na kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama msimu wa mapukutiko mwaka jana ambapo China ilikasirishwa na kitendo hicho na kufuta mikutano yote ya kibishara ilikuwa imepangwa baina ya viongozi wa China na Ujerumani.
Hatua ya kumalizika kwa mgogoro huo wa mahusiano kati ya China na Ujerumani imetangazwa na msemaji wa Kansela Angela Merkel ambaye alisema imekuja baada ya kansela Merkel kuzungumza kwa njia ya simu na waziri mkuu wa China Wen Jiabao.