1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz ahimiza mshikamano kuelekea mwaka mpya 2023

John Juma Mhariri: Zainab Aziz
31 Desemba 2022

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema vita vya Urusi nchini Ukraine ni "mtihani mgumu kwetu na nchi yetu." Amepongeza juhudi za umma mnamo wakati kuna mgogoro wa nishati na amesema Ujerumani haitasalitiwa.

https://p.dw.com/p/4Lb6Y
SPERRFRIST BEACHTEN | Berlin | Aufzeichnung der Neujahrsansprache von Bundeskanzler Scholz
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kwenye hotuba yake ya mwaka mpya, Kansela Olaf Scholz amewahimiza Wajerumani kuendeleza "mshikamano, nguvu… na ujasiri" ambao wamedhihirisha katika mwaka wa 2022 hata wanapoingia mwaka mpya wa 2023.

Aliyasema hayo kwenye hotuba ya mwaka mpya itakayopeperushwa kikamilifu kwenye runinga usiku wa Jumamosi, lakini ambayo ilikabidhiwa shirika la habari la DW mapema.

Scholz alibainisha kuwa 2022 ulikuwa "mwaka mgumu" lakini Ujerumani ilikuwa "nchi imara".

"Nchi inayofanya kazi kwa ukakamavu na utayari kwa mustakabali salama na imara,” alisema.

Amewataka Wajerumani kuendelea kushikamana katika mwaka ujao.

‘Tunawahurumia watu wa Ukraine'

Raia wa Ukraine akijaribu kuzima moto kwenye nyumba iliyoshambuliwa mjini Kherson.
Raia wa Ukraine akijaribu kuzima moto kwenye nyumba iliyoshambuliwa mjini Kherson.Picha: Igor Burdyga/DW

Mada iliyotawala hotuba ya Scholz ilikuwa vita vya Urusi nchini Ukraine.

Ulaya yaidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Urusi kutokana na kuivamia Ukraine

"Wengi wana wasiwasi kuhusu vita nchini Ukraine. Tunawahurumia watu wa Ukraine ambao hata katika siku kama leo, hawana amani kutokana na mashambulizi ya Urusi kwa makombora na roketi,” alisema.

Aliongeza kuwa "lakini historia ya mwaka 2022 haihusu vita pekee, mateso na hofu.” Waukraine wanailinda nchi yao, "tunashukuru kwa msaada wetu… na tutaendelea kuisaidia Ukraine,” aliapa.

Katika viwango vya utoaji misaada kwa Ukraine, Ujerumani inashikilia nambari ya pili baada ya Marekani. Imeipa Ukraine msaada wa zana za kivita zenye thamani ya mabilioni yad ola na vilevile misaada ya kiutu na kifedha.

Mshikamano wa Umoja wa Ulaya na NATO

Ujerumani inshika nambari ya pili kwa utoaji misaada kwa Ukraine baada ya Marekani.
Ujerumani inshika nambari ya pili kwa utoaji misaada kwa Ukraine baada ya Marekani.Picha: Diehl Defence/abaca/picture alliance

Scholz aliongeza kuwa Umoja wa Ulaya pamoja na Jumuiya ya Kujihami ya NATO zitaendelea kushirikiana pamoja kuliko namna ambavyo zimewahi kushikamana.

Scholz: Ulaya na Ujerumani zimeungana kuisaidia Ukraine

Ujerumani iliwapokea zaidi ya wahamiaji milioni moja kutoka Ukraine tangu Urusi ilipoivamia nchi yao Februari 24.

"Kutoa misaada katika hali ya dharura kama hiyo, ndiko hutufanya tuwe tulivyo, Hufanya nchi yetu taifa linalothamini utu na ubinadamu,” amesema Scholz.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa vita hivyo vimesababisha nyakati kuwa ngumu na vilevile ni mtihani mgumu kwao na kwa taifa lao.

"Katika maisha yetu ya kila siku, tunahisi na tunakabiliwa na athari za vita, mfano bei za juu za bidhaa madukani, bei ya juu ya mafuta, n ahata tunapolipia umeme au gesi,” amesema.

Lakini amesema nchi yake imekataa kuhujumiwa, badala yake imeendelea kushikamana Zaidi kuliko hapo awali.

Maoni: Mwaka mmoja wa Scholz uongozini, sifa zapiku ukosoaji

Mipango ya serikali kutoa ruzuku

​​​​Miongoni mwa miradi ya ruzuku ya serikali ya Ujerumani inalenga kuwasaidia wakaazi kumudu bei ya nishati.
​​​​Miongoni mwa miradi ya ruzuku ya serikali ya Ujerumani inalenga kuwasaidia wakaazi kumudu bei ya nishati.Picha: Ina Fassbender/AFP/Getty Images

Scholz alitaja juhudi za serikali yake kuweka akiba ya gesi kabla ya majira ya baridi kali na vilevile kutanua wanaowauzia nishati.

Aidha aliangazia ujenzi wa vituo vya gesi owevu, ambapo alikifungua kimoja mapema mwezi Disemba.

"Kutokana na juhudi hizi, tunaifanya nchi ye tuna Ulaya kutoitgemea gesi ya Urusi kwa muda mrefu,” alisema.

Scholz aliwapongeza Wajerumani kwa kutumia nishati kwa kiasi kidogo. Amewahimiza vilevile kuendelea na harakati hizo za kuhifadhi nishati.

Alitaja miradi mingine kadhaa ya serikali ya kumwezesha kila mkaazi wa Ujerumani kuweza kukabiliana na ongezeko la bei ya bidhaa.

Kansela Scholz alikariri kuwa mshikamano wa Ujerumani ni jambo la thamani kubwa.

"Tuendelee kufuata mkondo huo tulioanza mwaka uliopita. Tuufuate kwa ujasiri.”

Chanzo: DW