1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Scholz aishinikiza China juu ya uvamizi wa Urusi Ukraine

16 Aprili 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amemwambia mwenyeji wake, Rais wa China Xi Jinping kwamba uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unatishia usalama wa ulimwengu.

https://p.dw.com/p/4erHk
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na Rais wa China Xi Jinping
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na Rais wa China Xi JinpingPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kauli hiyo ya Scholz leo ni kama wito kwa China kuiwekea Urusi shinikizo zaidi na kufunga ushirikiano wao wa kimkakati ili kusuluhisha mgogoro huo.

Kulingana na taarifa fupi iliyotolewa na ofisi yake baada ya kukutana na Rais Xi, Scholz pia alisema hakupaswi kuwa na hata kitisho cha matumizi ya silaha za nyuklia kwenye vita hivyo ambavyo vimedumu kwa miaka miwili sasa.

Soma pia:Scholz akutana na Rais Xi siku ya mwisho ya ziara yake China

Mwezi uliopita, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitahadharisha kwamba serikali yake iko tayari kutumia zana za nyuklia ikiwa mamlaka yake au uhuru wa nchi yake utatishiwa.