1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani asema NATO haitajiingiza Ukraine

27 Februari 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema hakutakuwa na wanajeshi wowote wa ardhini kutoka Jumuiya ya Kujihami NATO, watakaopelekwa nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4cxVv
Olaf Scholz nchini Ufaransa na Emmanuel Macron
Ujerumani na Ufaransa zimekuwa zikipishana kauli katikasiku za karibuniPicha: Gonzalo Fuentes/AP/picture alliance

Akizungumza katika mji wa kusini magharibi mwa Ujerumani Freiburg, na akiuzungumzia mkutano wa Paris uliofanyika jana Jumatatu, ambako maafisa wakuu kutoka zaidi ya mataifa 20 walijadili namna ya kuiunga mkono zaidi Ukraine, Scholz amesema kile walichokianzisha na kukubaliana kuanzia mwanzoni ndicho kitakachoendelea kuwepo katika siku za usoni.

"Bila shaka tulijadili pia namna ya kuiunga mkono Ukraine, na kwa mjadala uliokwenda vizuri kabisa tulisema kile tulichokubaliana kuanzia mwanzo ndio tutakachokiendeleza, ikiwemo kutotuma wanajeshi wa ardhini, hakutakuwa na mwanajeshi yoyote katika ardhi ya Ukraine watakaotumwa huko na mataifa ya Ulaya au hata NATO na kwamba wanajeshi wanaofanya kazi kutoka mataifa yetu hawashiriki moja kwa moja katika vita hivyo," alisema Scholz.

Soma pia: Scholz: Uamuzi wa EU unapaswa kuwa ishara pia kwa Putin

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg amethibitisha kuwa hana nia ya kupeleka wanajeshi wake Ukraine.

Hata hivyo, Urusi imeonya uwepo wa mgogoro wa moja kwa moja kati ya NATO na Urusi hautaepukika iwapo muungano huo wa kijeshi itapeleka wanajeshi wake nchini Ukraine.