SiasaAsia
Scholz: Majaribio ya silaha za nyuklia yanatishia usalama
21 Mei 2023Matangazo
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema majaribio ya makombora ya nyukilia na yale ya masafa marefu ya Korea Kaskaziniyanatoa ishara ya uwepo wa kitisho cha usalama katika Rasi ya Korea.
Soma zaidi:Korea Kaskazini yafanya jaribio la chombo kinachoweza kushambulia chini ya bahari
Scholz, ambaye anazuru Korea Kusini baada ya kuhudhuria mkutano wa kilele wa G7 huko Hiroshima, Japan, pia aliitaka Korea Kaskazini kuacha kufanya majaribio ya kombora ya masafa marefu, na kusema kitendo hicho ni "tishio kwa amani" katika eneo hilo.
Kansela Scholz wa ametoa tauli hiyo baada ya baada ya kutembelea eneo lisilo na shughuli za kijeshi, (DMZ) linalotenganisha Korea Kaskazini na Korea Kusini.