Mafunzo
Karandinga: Upotevu Mjini Pyto
4 Machi 2020Matangazo
Akiwa na miaka 21, Tayo Shegun anakumbana na changamoto kubwa katika kazi yake ya kwanza: Anasimamia mageuzi ya ukataji mkaa kwenye mji wake wa Pyto, kituo kikuu cha ukataji na uchomaji mkaa nchini. Serikali imetoa mwongozo mpya kuifanya sekta hiyo iepukane na uharibifu wa mazingira na uwazi zaidi katika utendaji ili kupunguza msongamano na kudhibiti biashara ya magendo hasa na Ulaya. Mambo yanabadilika ghafla na kuwa mabaya wakati mjomba wake Felix, mwenyekiti wa Chama cha Wachoma Mkaa, anapotoweka. Anatuhumiwa kuiba mkaa wote kwenye mji huo, ambao ulikuwa umehifadhiwa na shirika la Tayo. Candice, anayesimamia mazingira na Jerome, diwani anayehusika na masuala ya mazingira wanaahidi kuupata ukweli. Je ni kweli Felix mwizi wa mkaa?