JamiiNigeria
Karibu watu 27 wafa maji baada ya boti kuzama, Nigeria
30 Novemba 2024Matangazo
Msemaji wa Idara inyosimamia masuala ya dharura kwenye jimbo la Kogi, Sandra Musa amesema, idadi jumla ya watu waliokufa itatolewa baada ya zoezi la uokozi kufungwa.
Amesema hadi sasa miili 27 imepatikana kufuatia ajali hiyo iliyotokea siku ya Alhamisi usiku na kazi ya kuwasaka wahanga inaendelea.
Boti hiyo kwa kiasi kikubwa ilikuwa imewabeba wafanyabishara wa jamii ya Missa, jimbo la Kogi waliokuwa wakielekea kwenye soko la wiki katika jimbo jirani la Niger na hawakuwa wamevaa vifaa vya kujiokoa, hali iliyosababisha wengi kuzama majini.