1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachimbaji saba wauliwa na wanajeshi nchini Ghana

20 Januari 2025

Chama cha wachimbaji wadogo wa madini nchini Ghana kimesema, wanajeshi waliwaua watu tisa wasio na silaha katika mgodi wa Anglo-Gold Ashanti nchini humo.

https://p.dw.com/p/4pMzY
Msumbiji Manica |Machimbo ya dhahabu
Machimbo ya dhahabbu huko Manica nchini MsumbijiPicha: Bernardo Jequete/DW

Kofi Adams ambaye ni mwenyekiti wa mkoa wa Chama cha Kitaifa cha wachimbaji wadogo Ghana amealiambia shirika la habari la Reuters kuwa watu tisa wameuawa wakiwa hawana silaha na wengine kumi na nne wamejeruhiwa vibaya katika tukio hilo lililofanyika katika eneo la uchimbaji dhahabu la Obuasi katika mkoa wa Ashanti.

Hapo awali, jeshi la Ghana lilisema kuwa takriban wachimba migodi 60 walikuwa wamebeba bunduki na silaha zingine kinyume cha sheria kwamba walivunja uzio wa mgodi na kuwashambulia kwa risasi timu ya wanajeshi iliyotumwa huko na kupelekea kuanza kurushiana risasi.

Tayari rais wa Ghana John Dramani Mahama ameamuru uchunguzi wa haraka ufanyike juu ya tukio hilo na kuwataka mamlaka ya mgodi huo wa Anglo-Dold Ashanti kushughulikia gharama za matibabu kwa majeruhi na gharama za mazishi.