1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres aonya dunia yarudi nyuma kuheshimu haki za binadamu

Hawa Bihoga
27 Februari 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa dunia imerudi nyuma katika kuheshimu haki za binadamu, na kutoa wito wa kuhuishwa kwa Tangazo la Kimataifa ya Haki za Binadamu, miaka 75 tangu kusainiwa kwake.

https://p.dw.com/p/4O2HT
Schweiz | Sitzung UN Menschenrechtsrat in Genf | Antonio Guterres
Picha: Benoit Doppagne/Belga/dpa/picture alliance

Antonio Guterres ametoa onyo katika ufunguzi wa kikao cha mwaka cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjni Geneva. 

Akigusia vita vinavyoendelea nchini Ukraine, njaa na majaga ya tabianchi, Guterres amesema tangazo hilo lilikuwa linakabiliwa na kile alichokiita mashambulizi kutoka pande zote.

Guterres: Haki za binaadamu zinadhoofishwa na vita

Amesema uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umesababisha ukiukaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu unaoshuhudiwa duniani. 

Wakati dunia imepiga hatua kubwa katika haki za binadamu na maendeleo ya binadamu, Guterres ameonya kuwa mizozo hiyo badala ya kuendeleza maendeleo hayo, imerudisha nyuma.