Kenya kuelekea uchaguzi mkuu 2022
Zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi mkuu nchini Kenya utakaofanyika Agosti 9. Wakenya watakuwa na fursa nyingine ya kikatiba kumchagua kiongozi mpya wa taifa hilo.
Wagombea wakuu katika uchaguzi mkuu wa Kenya
Raila Odinga wa muungano wa Azimio la Umoja Kenya na naibu rais William Ruto wa muungano wa Kenya Kwanza ndio wagombea wakuu katika uchaguzi wa 2022 nchini Kenya.
Tume ya IEBC iko tayari kwa uchaguzi mkuu
Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya Wafula Chebukati ametoa hakikisho kwamba maandalizi yanaendelea vizuri na tume hiyo iko tayari kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 9
Mdahalo wa wagombea urais
Mdahalo wa wagombea urais ulisusiwa na wagombea wengine na kuhudhuriwa tu na naibu rais William Ruto
Usalama waimarishwa
Maafisa wa usalama, viongozi wa kidini na kijamii, washirikiana kuhakikisha amani na mshikamano kabla, wakati na baada ya uchaguzi
Kampeini zapamba moto
Wagombea urais wanazuru maeneo mbalimbali kutafuta uungwaji mkono kabla ya siku ya mwisho ya kampeni. Umati mkubwa hapo umejitokeza kumpigia debe Raila Odinga wa muungano wa Azimio la Umoja
Kampeni zanoga
Wafuasi wa naibu rais William Ruto mgombea wa muungano wa Kenya Kwanza pia wajitokeza kwa wingi kumpigia debe mgombea wao
Mkenya wa kawaida
Matarajio ya Mkenya wa kawaida ni yapi kutoka kwa wagombea hasa wakati huu ambapo taifa hilo linakumbwa na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama ya maisha?
Rais anayeondoka madarakani
Rais Uhuru Kenyatta anaondoka madarakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili na ameweka nguvu zake nyuma ya mgombea urais Raila Odinga wa muungano wa Azimio la Umoja