Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itapeleka wanajeshi katika eneo la kaskazini mwa nchi ambalo limekumbwa na ukame na kuwatuhumu majambazi na wezi wa mifugo kwa kuwaua watu wengi. Sikiliza mahojiano ya Sylvia Mwehozi na mchambuzi wa masuala ya usalama Kenya George Musamali akianza kueleza madhara ya amri hiyo.