1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yawaondoau wanaoishi katika msitu wa Mau

Angela Mdungu
19 Agosti 2019

Serikali ya Kenya imeanza utaratibu wa awamu ya pili ya kuwaondoa watu wanaoishi katika Msitu wa Mau kwa minajili ya uhifadhi wa chemchem zilizomo kwenye msitu huo muhimu

https://p.dw.com/p/3O7AP
Kenia Frau mit Bambusstangen
Picha: picture-alliance/dpa/S. Morrison

Waziri wa mazingira wa Kenya ameeleza kuwa wakati huu wanawakusudia wamiliki wa mashamba makubwa msituni humo pamoja na takribani hatimiliki 1,200 zinazoaminika kuwa sio halali. Wanaharakati wa mazingira wanaunga mkono juhudi hizi ila wanahimiza suluhu ya kudumu wakihofia uhalifu katika zoezi hili.

Serikali ya Kenya imeanza harakati za kuwaondosha watu kutoka msitu wa Mau kwa minajili ya uhifadhi wa msitu huo wakati huu zoezi hili likiwalenga wamiliki wa mashamba makubwa. Hii ni awamu ya pili na waziri wa mazingira Keriako Tobiko amefanya mkutano na maafisa wa usalama pamoja na maafisa wa huduma ya misitu huko Narok.

Haya yanajiri baada ya serikali kuchapisha katika magazeti kuwa takriban hatimiliki 1,274 za ardhi zitabatilishwa. Mwanaharakati wa mazingira na haki za binaada Joseph Towett  amesema hii ni hatua muhimu hasa ikizingatiwa kuwa wamiliki wakubwa wa mashamba katika misitu hiyo ni wanasiasa walio na ushawishi mkubwa:

Mwaka 2013 siasa kuhusu kuwafurusha watu katika msituni wa Mau ili kuuhifadhi lilimnyima kura kiongozi wa ODM Raila Odinga baada ya wakaazi wa eneo hilo kumpa uungwaji mkono mkubwa mwaka 2007. Wakati huo naibu rais Wiliam Ruto alizipiga vita juhudi zake za uhifadhi wa msitu huo.

Hata hivyo waziri Tobiko ameapa kuwa hakuna litakalositisha zoezi hili. Awamu hii ya pili inalenga kuwafurusha watu elfu 60, baada ya awamu ya kwanza iliyowaondoa watu elfu 10.

Wakio Mbogho/ DW Nakuru