1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Biashara

Kenya yaigeukia UAE kwa mikopo baada ya China kujitoa

15 Januari 2025

Kenya imeanza mazungumzo na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE kupata fedha za kusimamia shughuli ya kukamilisha ujenzi wa reli yake.

https://p.dw.com/p/4pAyz
Kenia Nairobi | Vereidigungszeremonie Vize-Präsident Kithure Kindiki
Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Rais William Ruto ametangaza hatua hiyo baada ya China kukata ufadhili wa kusimamia ujenzi wa miradi ya miundo mbinu. Ujenzi wa reli inayounganisha bandari ya Kenya ya Mombasa na mataifa jirani yasiyokuwa na bandari, kama sehemu ya mradi ulioanzishwa na China wa ujenzi wa miundo mbinu ya reli na barabara, uliishia katika eneo la Bonde la Ufa mnamo mwaka 2019 baada ya Beijing kuondoa ufadhili wake.

Soma: Kenya, EU wakaribia kukamilisha makubaliano ya biashara

Ruto amesema katika ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa X, kwamba wanatafuta makubaliano ya kushirikiana na Umoja wa Falme za Kiarabu kuendeleza ujenzi huo wa reli hiyo ya kisasa kuziunganisha Kenya, Uganda na Sudan Kusini. Ujumbe huo wa Ruto ameuandika jana usiku baada ya mazungumzo yake na maafisa wa UAE mjini Abu Dhabi.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW