JamiiHaiti
Kenya yasimamisha mpango wa askari wake kwenda Haiti
13 Machi 2024Matangazo
Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry kukubali kujiuzulu huku magenge yenye silaha yakidhibiti sehemu kubwa ya taifa hilo la Caribbean.
Katibu katika wizara ya mambo ya kigeni ya Kenya Korir Sing'oei amenukuliwa na AFP akisema "Kumekuwa na mabadiliko ya makubwa ya hali kutokana na kutokuwepo kwa utawala wa sheria na kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Haiti."
Hata hivyo Sing'oei amesema Kenya imesalia kujitolea "kutoa uongozi kwa MSS," akimaanisha ujumbe wa Msaada wa Usalama wa Kimataifa ambao uliidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Oktoba mwaka jana.