Kenya yazindua reli ya kisasa
31 Mei 2017Treni yenye rangi nyeupe na nyekundu iliondoka katika kituo chake cha kwanza katika mji wa pwani wa Mombasa, ikimchukuwa Rais Kenyatta na maafisa kadhaa wa serikali ya China pamoja na raia wa kawaida katika safari hiyo ya kwanza kwenda mji mkuu, Nairobi.
Awali safari ya Mombasa-Nairobi iligharimu kiasi cha masaa matano, lakini kwa usafiri huu mpya na wa kisasa, sasa itachukuwa nusu ya muda huo kusafiri kati ya miji hiyo.
Kawaida, safari hii hapo kabla ilikuwa inafanyika katika reli moja na kusababisha ajali na watu wengi kupoteza maisha.
Ikijulikana kama 'Madaraka Express', treni hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 1,260 na kuchukua nafasi ya kile kilichojulikana kama 'Reli ya Wendawazimu' iliyojengwa zaidi ya karne moja iliyopita na wakoloni wa Kiingereza, ambayo inafahamika kwa kuchelewesha sana kwenye safari zake.