1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSaudi Arabia

Kesi dhidi ya bin Salman kuhusu mauaji ya Khashoggi yafutwa

7 Desemba 2022

Jaji mmoja nchini Marekani ameitupilia mbali kesi dhidi ya Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman kuhusiana na mauaji ya mwaka wa 2018 ya mwandishi habari Jamal Khashoggi.

https://p.dw.com/p/4Kaul
Saudi-Arabien Riad | Mohammed bin Salman
Picha: Balkis Press/ABACAPRESS/picture alliance

Jaji John Bates amezungumzia kile alichokiita wasiwasi kuhusiana na uamuzi wake lakini akasema ilimbidi kufuata pendekezo la karibuni la Wizara ya Sheria ya Marekani kuwa bin Salman apewe kinga ya kushitakiwa.

Wasiwasi wa Bates ulitokana sio tu na tuhuma za kuaminika za kuhusika kwa mwanamfalme huyo katika mauaji ya Khashoggi, lakini pia na wakati wa uteuzi wa bin Salman kuwa waziri mkuu wa Saudi Arabia.

Kesi hiyo iliwasilishwa na mchumba wa Khashoggi, Hatice Cengiz, ambaye anamtuhumu Rais wa Marekani Joe Biden kwa kumpa kinga bin Salman.