1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya mauaji ya balozi wa Italia yaendelea kusikilizwa

8 Machi 2023

Waendesha mashitaka katika kesi ya watu sita waliotuhumiwa kwa kumuuwa balozi wa Italia nchini Kongo mwaka wa 2021 wameomba adhabu ya kifo kwa watuhumiwa hao wakati kesi hiyo iliposikilizwa leo mjini Kinshasa.

https://p.dw.com/p/4OPH3
DR Kongo | Luca Attanasio, ermordeter italienischer Botschafter
Picha: FOTOGRAMMA/IPA/picture alliance

Waendesha mashitaka katika kesi ya watu sita waliotuhumiwa kwa kumuuwa balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka wa 2021 wameomba adhabu ya kifo kwa watuhumiwa hao wakati kesi hiyo iliposikilizwa leo mjini Kinshasa. Luca Attanasio, balozi wa zamani wa Italia nchini Kongo, alikuwa miongoni mwa watu watatu waliouawa mnamo Februari 22, 2021, wakati msafara wa Umoja wa Mataifa ulivamiwa katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Wengine waliouawa ni dereva Mustapha Milambo na afisa wa polisi wa Italia Vittorio Iacovacci. Mahakama ya kijeshi inayochunguza mauaji hayo ilifunguliwa mjini Kinshasa Oktoba. Kongo kimsingi haijakuwa ikitekeleza adhabu ya kifo tangu mwaka wa 2003, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, lakini mahakama zinaendelea kutoa hukumu hiyo.