Kesi ya Radovan Karadzic
2 Machi 2010Kiongozi wa zamani wa Waserbia wa Bosnia, Radovan Karadzic amevielezea vita vya Bosnia vya miaka ya 1990, kama vita vitakatifu vilivyofanywa na Waserbia dhidi ya Waislamu waliokuwa wanataka kuigeuza Bosnia kuwa jamhuri ya Kiislamu.
Kauli hiyo ameitoa jana katika mahakama ya kimataifa ya The Hague na alidai kuwa analitetea taifa lake na sio yeye mwenyewe. Karadzic ameiambia mahakama hiyo kuwa uongozi wa Kiislamu wa Bosnia kwa wakati huo ulikua na hatia ya kuanzisha uadui kwa kukataa mpango wa kugawana madaraka.
Ameongeza kuwa kila kitu kilichofanywa na Waserbia kama sehemu ya kujitetea kwao mahakama ya Umoja wa Mataifa inakichukulia kama kosa la uhalifu. Karadzic hana wakili na anajitetea mwenyewe katika mahakama hiyo iliyopo nchini Uholanzi.