Kesi ya udanganyifu wakati wa COVID yasikilizwa Ujerumani
11 Agosti 2023Wanaume hao, kupitia kutumia kampuni bandia wanadaiwa kufungua vituo 10 vya kupimia virusi vya korona, katika miji ya Cologne na Langenfeld waliilidanganya shirika la umma la bima ya afya la Nordrhein na kulipwa fedha hizo.
Kulingana na mwendesha mashitaka watuhumiwa hao waliamua kujinufaisha kupitia mchakato wa malipo ambao haukuwa na urasimu mwezi Juni 2021 na kudai malipo hayo kwa shirika hilo la bima ya afya.
Walifungua akaunti za mtandaoni kwa kutumia majina ya watu wengine ambao raia wa Italia kwa ajili ya malipo ya vituo hivyo ambavyo havipo.
Walifanya hivyo kwa kudai malipo ya vipimo ambavyo havikuwahi kufanyika. Walitumia namba za vituo vingine vilivyoandikishwa kudai malipo.
Mshtakiwa wa tatu kwenye kesi hiyo anadaiwa kusaidia uhalifu huo kwa kuweka masanduku ya barua ya vituo hivyo bandia mitaani. Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa kwa mara nyingine kumi na saba na hukumu inatarajiwa kusomwa mwisho wa mwezi Oktoba