1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Annan aionya Sudan kuhusu mgogoro wa Darfur

6 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDF2

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan ameionya serikali ya Sudan kuwa itawajibika kwa mzozo wa kibinadamu unaozidi kuwa mbaya katika jimbo la Darfur.Annan ametamka hayo siku moja baada ya vikosi vya amani vya Umoja wa Afrika kusema kuwa vitapaswa kuondoka Darfur kwa sababu serikali ya Khartoum imekataa kuviruhusu vikosi hivyo kuwa chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa.Sudan imelikataa azimio lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,kuunda kikosi cha kimataifa cha wanajeshi 20,000 kuwapokea wanajeshi wa Umoja wa Afrika,tarehe 30 mwezi wa Septemba.Si chini ya watu 200,000 wameuawa katika mgogoro wa Darfur na hadi watu milioni 2.4 wamepoteza makazi yao tangu mapigano kuanza miaka mitatu na nusu iliyopita.