1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Annan asema Darfur inahitaji misaada zaidi

29 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF90

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan akikamlisha ziara yake ya siku tatu nchini Sudan,amelitembelea eneo la kusini nchini humo.Annan anajitahidi kuyapa nguvu makubaliano ya amani yaliotiwa saini mwezi wa Januari kati ya serikali ya Sudan na waasi kusini mwa nchi.Makubaliano hayo,yamemaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 21 kati ya pande hizo mbili.Lengo la ziara ya Annan nchini Sudan ni kuhimiza juhudi za kiutu na usalama katika jimbo la magharibi la Darfur na vile vile kuimarisha mkataba wa amani kati ya serikali na waasi kusini mwa nchi.Siku ya Jumamosi Annan alitembelea kambi ya wakimbizi ya Kalma,ambayo ni kubwa kabisa katika jimbo la Darfur.Baadae aliwaambia maripota kuwa amehuzunishwa sana na yale aliyoona.Akasema, misaada zaidi inahitajiwa ili kuweza kupambana na matatizo ya jimbo la magharibi la Darfur na vile vile kusini mwa Sudan.